Rapa anaeiwakilisha Ilala, Chidi Benz ameweka wazi kuwa yuko katika wakati mgumu na anahitaji msaada kutokana na yanayomsibu.

Akiongea na Da Weekend Chat Show ya Clouds TV hivi karibuni, Chid Benz amesema kuwa bado ana uwezo mkubwa wa kufanya muziki lakini wadau wa muziki wamempa kisogo kwa makusudi wakihofia kuwa akiwa kileleni kama zamani atawapoteza wasanii wengi wa hip hop walioko kileleni hivi sasa.

“Hawa Joh Makini sijui, nani wanakuwa hawapo. Sasa hakuna mdau anayeweza kukubali akina Joh Makini wasiwepo awepo Chidi Benz peke yake,” alisema.

Alisema kuwa hali yake sasa imebadilika kwa kiasi kikubwa kwakuwa wakati alipokuwa kileleni alikuwa na uwezo wa kufanya shows kila wiki tofauti na ilivyo hivi sasa.

Akizungumzia chanzo cha kupungua kwa kasi kwa mwili wake, alisema kuwa msongo wa mawazo ni kitu kikubwa kinachopelekea awe katika hali anayoonekana nayo hivi sasa.

“Matatizo yangu na stress zangu ambazo niko nazo zinanisababishia mwili wangu unapungua kwasababu siko okay, siko poa, siko sawa yaani,” alieleza.

Amesema kuwa hivi karibuni mama yake mzazi alimshuhudia akifanya show ya saa mbili na alitoa machozi kutokana na jinsi alivyofanya vizuri na kupokelewa na mashabiki. Ndipo waliposhauriana kuwa ni vyema atafute watu wa kumsaidia ili aendelee kufanya muziki wake na kupata mafanikio.

“Mama yangu akaniambia mwanangu unafanya show two hours, show kali watu wanapenda unachokifanya lakini sioni mwamko wa watu kutokea kukusaidia, kwahiyo tufanye mpango watu wakusaidie. Na mimi namuambia nataka watu wanisaidie, natamani kusaidiwa, natamani kupata mafanikio anayopata Diamond,” alieleza kwa uchungu.

 

NEC yatangaza kusimamia uchaguzi wa Zanzibar ‘Kijitoupele’
Zanzibar: Mwandishi wa DW apotea uwanja wa Ndege