Mwanamziki wa bongo fleva aliyekuwa ametumbukia katika dimbi la utumiaji dawa za kulevya Chidi benzi licha ya kuripoti hapo awali ya kuwa ameachana na madawa ya kulevya na kurudi na ngoma yake mpya iitwayo chuma na kufanikiwa kupenya na huo wiimbo, chidi kaamua kurudia katika matumizi ya dawa za kulevya.
Mwana harakati wa kupambana na matumizi ya dawa za kulevya Kalama Masudi kwa jina la kisanii anajulikana kama Kalapina ameahidi kumtafuta kwa udi na uvumba chidi benzi ili amrudishe tena sober house,na kusema kuwa hii ndiyo itakuwa mara yake ya mwisho kumsaidia ,”hii itakuwa mara yangu ya mwisho kumsaidia akirudi tena nitamuacha kwa kuwa namuona chidi ana kitafuta kifo kwa nguvu kwa kuwa madawa ya kulevya anayo tumia chidi benzi au chidi chuma ni makali sana”Alisema Kalapina.