Timu ya Taifa ya Chile inatarajiwa kuumana na Timu ya Taifa ya Ureno katika michuano ya kombe la mabara inalofanyika nchini Urusi.

Aidha, katika michuano hiyo mikali inayoshirikisha timu za taifa za mabara, nahodha wa Timu ya Chile, Marcelo Diaz amesema kuwa watamdhibiti Cristian Ronaldo asiweze kufanya chochote katika mechi hiyo.

“Sote tunajuwa ni mchezaji mzuri, anauwezo wa kubadilisha matokeo wakati wowote na anamsimu mzuri na mchezaji bora, sisi tutamdhibiti katika mechi yetu hatoweza kufanya chochote,”amesema Diaz.

Hata hivyo, Ronaldo amekuwa gumzo kubwa mara baada ya kutojulikana kwa hatma yake katika klabu anayoichezea ya Real Madrid kama ataondoka na kuelekea Manchester United ama kubaki.

Dani Alves: Kwaheri Juventus FC
Mwanamuziki Bobi Wine aigeukia siasa, atiwa mbaroni