Mabingwa wa soka Tanzania bara Young Africans wameshindwa kuendelea kuonyesha ubabe baada ya kuondolewa katika michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa kufungwa kwa penati na URA ya Uganda.

Young Africans ambayo ilikuwa ikipewa nafasi ya kufanya vyema katika michuano hiyo kwa kufika fainali na ikiwezekana kitwaa ubingwa, imeishia hatua ya nusu fainali baada ya kufungwa kwenye Uwanja wa Amaan kisiwani unguja dhidi ya wapinzani wao, ambao pia waliiondoa Simba katika hatua ya makundi.

Hadi dakika za kawaida za mchezo zinakamilika matokeo yalikuwa suluhu ndipo mchezo huo uamuliwe kwa kupigwa mikwaju ya penati.

Young Africans walipata penati nne huku wapinzani wao wakipata tano, mchezaji wa Young Africans aliyekosa penati ni Obrey Chirwa ambaye ulikuwa ni mchezo wake wa kwanza kucheza baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda, kutokana na madai yake ya kimaslahi dhidi ya uongozi wa klabu hiyo.

Kutokana na matokeo hayo, URA wamefanikiwa kufuzu hatua ya fainali ambayo itachezwa Jumamosi, ikisubiri matokeo ya Azam FC dhidi ya Singida United.

Magazeti ya Tanzania leo Januari 11, 2018
Serengeti Lite yanogesha ligi ya wanawake,TFF,SBL wasaini mkataba

Comments

comments