Siku chache baada ya rapa Chid Benz kumtaka mkali wa mitindo ya kuimba, Chin Bees kubadili haraka jina kwa madai kuwa majina yao yanafanana, mwimbaji huyo amesema hatafuata matakwa hayo.

Chin Beez ambaye yuko chini ya lebo ya Wanene Entertainment, ameiambia E-News ya EATV kuwa hawezi kubadili jina hilo kwani majina hayo hayafanani na wanafanya muziki tofauti.

“Mimi siwezi kubadilisha jina kwa sababu ya Chid Benz kwa sababu halifanani, very different (tofauti sana). Mimi nafanya muziki wangu, siwezi nikakaa nipiganie jina. Hivyo, bro kama anahitaji jina dah!, sidhani kama jina langu linaendana na lake  ‘me am do my thing’ (mimi nafanya yangu),”  Chin Beez alifunguka.

Hivi karibuni, Chid Benz alimtaka mkali huyo wa ‘Pepeta’ kufanya mabadiliko hayo akidai kuwa yeye ni msanii mchanga mwenye hits zisizozidi saba ukilinganisha na makumi ya hits za kiongozi huyo wa ‘La Familia’.

Hata hivyo, tamko la Chid kwa Chin Bees huenda likawagusa zaidi wasanii wengi wachanga ambao wana majina yanayoanza na ‘Chid’ (mfano Chid Fenda), majina ambayo huyatumia majukwaani na kwenye kutambulisha nyimbo zao.

Magazeti ya Tanzania leo Julai 8, 2017
Roma: Ningesema mlichotaka kusikia ingekuwa mwisho wa muziki wangu