Kama ilivyo nchini Tanzania kuwa na tamasha la nyama choma basi nchini  China mwaka 2009 walianzisha tamasha la ulaji wa nyama za mbwa wakiamini kuwa nyama ya mbwa huongeza afya ya mwili na kukinga mwili dhidi ya magonjwa, lakini pia wakiamini nyama ya mbwa husaidia wapenzi kushiriki vyema tendo la ndoa.

Tamasha hilo linalofanyika kila mwaka na husherekewa takribani kwa siku 10 ambapo zaidi ya mbwa 10,000 hufanywa kitoweo, na mwaka huu linafanyika kuanzia juni 21 hadi Juni 30.

Tamasha hilo ni maarufu kama Yulin ambapo watu hujivinjari kwenye migahawa na masokoni kwa kula nyama ya mbwa kwa wingi.

Ulaji wa nyama ya mbwa nchini China umehalalishwa hali iliyopelekea takribani idadi ya mbwa milioni 10 hadi 20 kuliwa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.

Aidha tamasha hilo lilisemekana kutofanyika mwaka huu kwa kile kilichodaiwa kuwa mamlaka italizuia lakini mambo hayakuwa hivyo ijapokuwa hakuna shamra shamra katika tamasha hilo kama ya miaka iliyopita.

Taifa la China linatajwa kuwa kati ya mataifa ambayo Wanachi wake wanakula nyama ya mbwa kwa wingi duniani ingawa baadhi ya Wanaharakati wanapinga ulaji huo wa nyama ya mbwa kwa kile wanachokidai kuwa mbwa ni rafiki wa binadamu hivyo hastahili kugeuzwa kitoweo.

 

Neymar, Coutinho waibeba Brazil
Brazil, Nigeria yatawakuta ya Argentina leo?

Comments

comments