China imeridhia kutoa msaada wa dola za Marekani milioni 62 sawa na shilingi bilioni 138.3 za Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Usafirishaji  nchini.

Balozi wa China nchini, Wang Ke amesema hayo leo Jumatatu, Februari 12, muda mfupi baada ya kufanya mazungumzo na Rais John Magufuli na kumkabidhi barua yenye ujumbe wa Rais wa China, Xi Jinping, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Wang Ke ameeleza kuwa msaada huo ni sehemu ya misaada na miradi mbalimbali ambayo China inaitekeleza nchini Tanzania yenye lengo la kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati yake na Tanzania.

Kwa upande wake, Rais Magufuli amemuomba Wang Ke kumfikishia shukrani zake kwa Rais wa China kwa ujumbe na msaada huo ambao amesema utasaidia kuimarisha huduma za usafirishaji nchini.

Serikali kuimarisha mfumo wa utoaji huduma za madawa
Shinyanga wapunguza mauaji ya vikongwe