China imesema itachukua hatua “halali na muhimu” dhidi ya Marekani ili kujibu hatua ya hivi karibuni ya Marekani kuwawekea vikwazo maafisa wa China wanaotuhumiwa kwa ukiukwaji wa haki za binaadamu.

Marekani imeweka sheria ngumu kwa maafisa wa China na wanafunzi wa China kuingia nchini humo kama sehemu ya kampeni yake dhidi ya China, ambayo inaonekana kuwa adui wake mkubwa wa kimkakati katika siku za hivi karibuni.

Marekani pia imefuta vibali vya kuishi vya zaidi ya wanafunzi 1,000 wa China wanaoshukiwa kuwa majasusi.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo, amesema vikwazo hivo vinawalenga maafisa wa China wanaoaminika kuhusika na vitendo vya ukandamizaji wa uhuru wa dini, jamii ya walio wachache, wapinzani na hata makundi ya kutetea haki za binaadamu.

Hata hivyo, China kupitia Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje Wang Wenbin, imeishtumu Marekani kwa kuingilia kati mambo ya ndani ya China.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Desemba 23, 2020
Waziri Mkuu apigia chapuo sekta binafsi