Bendera ya Marekani imeteremshwa leo katika ubalozi mdogo wa China uliopo mjini Chengdu ikiwa ni siku chache tangu Beijing ilipoamuru kufungwa kwa ubalozi huo ikijibu hatua ya Marekani ya kuufunga ubalozi mdogo wa China mjini Houston.

Picha za video zilizorushwa na shirika la habari la utangazaji la China CCTV zimeonesha bendera ya Marekani ikiteremshwa mapema leo asubuhi baada ya kuzidi mvutano wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili.

Kila upande unaulaumu mwingine kwa kuhatarisha usalama wa taifa na mahusiano baina ya nchi hizo mbili yamepwaya katika siku za karibuni na kuchukua mkondo wa makabiliano ya enzi ya vita baridi.

Muda wa mwisho kwa Wamarekani kuondoka kutoka mji wa Chengdu bado haujulikani lakini wafanyakazi wa ubalozi mdogo wa Chini mjini Houston walipewa muda wa saa 72 kufunga ubalozi huo na kuondoka.

Polisi Tanzania kusajili wazawa
TFF kumpeleka Eymael FIFA