Aina mpya ya mafua ya nguruwe ambayo inaweza kuwa janga kubwa la kiafya imegunduliwa na Wanasayansi nchini China.

Kwa mujibu wa ripoti mpya ya 29 june, 2020 iliyotolewa na Proceedings of the National Academy of Sciences of United States of America (PNAS) wamependekeza kirusi hicho kiitwe jina la G4 EA H1N1 na kidhibitiwe mapema kwani inawezekana binadamu wana kinga mwili ndogo ya kupambana nayo au hawana kabisa.

Imeelezwa kuwa mafua hayo yapo kwa nguruwe lakini binadamu wanaweza kuambukizwa. Wanasayansi hao wana hofu kwamba yanaweza kusambaa kirahisi na kusababisha mlipuko.

Hata hivyo, Watafiti wamesema mafua hayo yanaweza yasiwe tatizo kwa sasa japokuwa suala hilo linahitaji uangalizi wa karibu kwasababu binadamu wanaweza kuambukizwa.

Tanzania yapokea mkopo wa Bil. 592.57
Waziri Kabudi adhihirisha nia kugombea ubunge Kilosa