China imeridhia kutoa msaada wa Dola za Marekani Milioni 62 sawa na shilingi Bilioni 138.3 za Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa Chuo kikuu cha Usafirishaji hapa nchini.

Balozi wa China hapa nchini, Wang Ke amesema hayo leo pindi alipokuwa akifanya mazungumzo na Rais John Pombe Magufuli na kumkabidhi barua yenye ujumbe wa Rais wa China, Xi Jinping, Ikulu Jijini Dar es salaam.

Wang Ke ameeleza kuwa msaada huo ni sehemu ya msaada na miradi mbalimbali ambayo China inaitekeleza hapa nchini Tanzania yenye lengo la kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati yake na Tanzania.

Kwa upande wake Rais Magufuli amemuomba Wang Ke kumfikishia shukrani zake kwa Rais wa China kwa ujumbe na msaada huo ambao amesema utasaidia kuimarisha huduma za usafirishaji hapa nchini.

 

Video: Hakuna maisha magumu kama kuishi kinafiki- Bashe
Video: Tanzania ni kitovu cha ukombozi wa Bara la Afrika- Dkt. Mwakyembe