China imeipiga marufuku Marekani kutumia anga lake kufanya uchunguzi wa silaha za nyuklia dhidi ya Korea Kaskazini mara baada ya kuidhibiti ndege ya kufanya uchunguzi kutoka Marekani liliyokuwa inatumia anga la nchi hiyo.

Aidha, ndege hiyo ilitumwa kwa ajili ya kufanya uchunguzi dhidi ya mionzi ya silaha za nyuklia yaliyofanywa na Korea Kaskazini ambapo baada ya ndege hiyo kuingia anga la China ilishushwa mara moja na ndege za kijeshi za China.

 

Ikizungumzia hatua hiyo iliyochukuliwa na China, Marekani imesema kuwa China imetumia nguvu kubwa kuishusha ndege hiyo kwani ilikuwa katika doria ya kwaida katika shughuli za kijeshi za anga.

Hata hivyo, China imeonya hatua hiyo ya Marekani kuwa inaweza kuhatarisha mahusiano ya kidiplomasia baina ya nchi hizo. kwani kuingilia anga la nchi hiyo bila taarifa ni kufanya makosa

Ndege za China zaipiga 'mkwara mkali' ndege ya kivita ya Marekani
Watu 60 wauawa katika mapigano makali Libya