Watunga Sera wa China wanajadili namna bora zaidi ya kumng’oa Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un na jeshi linalomtii kufuatia maandalizi  yake ya kufanya jaribio la sita la makombora ya nyukilia.

china-na-kim-jung-un

Korea Times imemkariri Profesa Zhe Sun ambaye ni mhadhiri wa chuo kikuu na mtaalam wa Mipango na Sera wa China akisema kuwa wapanga sera wa nchi hiyo wanajadili mbinu ikiwa ni pamoja na kuungana na Marekani na Korea Kusini kumuondoa kijeshi kiongozi huyo.

“Baadhi ya wasomi na watunga sera wa China wameanza mazungumzo ikiwa ni pamoja na kuunga mkono  oparesheni ya kijeshi ya Marekani na Korea Kusini ya kumng’oa Kim Jong-Un,” alisema Profesa Zhe Sun.

Korea Kusini inajiandaa kufanya jaribio la sita la bomu la nyuklia tangu ilipofanya jaribio la kwanza mwaka 2006, jaribio ambalo litakuwa la tatu kwa mwaka huu huku likitishia usalama wa dunia hususan mahasim wa nchi hiyo, Marekani na Korea Kusini.

Marekani na Korea Kusini wamekuwa wakitishia kuanzisha mashambulizi ya kijeshi kulenga maeneo yenye vinu vya nyuklia vya Korea Kaskazini.

Ali Kiba ajiachia na Raila Odinga Mombasa
ATCL yataja tarehe rasmi ya kuruka na nauli za ndege mpya