China imekumbwa na maporomoko ya udongo ambapo watu zaidi 140 wanahofiwa kufukiwa katika jimbo la Sichuani lililopo magharibi mwa nchi hiyo ambapo ndiyo sehemu iliyoathirika pakubwa na maporomoko hayo.

Inahofiwa kuwa zaidi ya nyumba 40 zimefukiwa na maporomoko ya udongo katika kijiji cha Xinmo Maoxian mara baada ya upande mmoja wa mlima kuporomoka na kusababisha maafa hayo.

Aidha, katika taarifa iliyotolewa na maafisa wa polisi katika Shirika la Utangazaji la China CCTV imesema kuwa maporomoko hayo yamesababishwa na mvua kali ambazo zimekuwa zikinyesha maeneo hayo.

Vanessa Mdee afunguka kuhusu kupigana chini na Jux
Wizara ya maliasili na utalii kutoza kiingilio sabasaba