China imesema makubaliano ya muda yamefikiwa na uongozi wa Vatican juu ya kuteuliwa kwa maaskofu na kufungua ukurasa mpya kati ya mahusiano ya China na Vatican baada ya mgogoro wa kipindi kirefu uliokuwa kati ya nchi hizo.

Katika maoni yaliyowekwa katika tovuti yake, China imelitambua rasmi kanisa Katoliki, na kusema kwa moyo mkunjufu imewaafiki na wamesaini mkataba ulioitwa mkataba wa kiuchungaji na siyo kisiasa na kuahidi kuendelea kufuata njia inayowafikia na jamii ya kisoshalisti, chini ya uongozi wa Chama Cha Kikomunisti Cha China (CCP).

Lakini, idadi ya Wakatoliki milioni 12 wanaokadiriwa kuwapo nchini China, wamegawanyika juu ya mkataba huo, wakati kanisa lisilo rasmi likiwa linamfuata Kiongozi wa Kanisa Katoliki, Kadinali mstaafu wa Hong Kong Joseph Zen ambaye amekataa makubaliano hayo na kusema ni usaliti uliyo fanywa na Vatican.

Brian Lucas ni Mkurugenzi wa Taifa wa Taasisi ya Kikatoliki, ambayo ni Jumuiya ya misaada ya Wakatoliki ya Australia amekiambia chombo cha habari cha VOA kuwa suala hili limekuwa gumu na maoni ya pande zote mbili za wale wanaounga mkono makubaliano hayo na wale wanaokosoa wanachukulia kuwa ni jambo jepesi.

Vatican tayari imewatambua maaskofu kadhaa walio teuliwa na serikali ya China.

Katika tamko lake, Vatican imesema kuwa mkataba huo “ni matunda ya maridhiano ya pande mbili ya hatua baada ya hatua,” na wanatarajia itapelekea kuwepo muungano wa Wakatoliki wote nchini China.

Daniel Cousin kocha mpya The Panthers
Pape Cheikh Gueye asubiri wito wa Luis Enrique