Bunge la China limepitisha mabadiliko ya Katiba na kuondoa ukomo wa muda wa urais ambao awali ulikuwa mihula miwili. Mabadiliko hayo yanampa nafasi Rais Xi Jinping kuendelea na urais bila ukomo.

Bunge limepiga kura leo na kupitisha kwa kishindo mabadiliko hayo. Ni wabunge wawili pekee waliopiga kura ya kupinga mabadiliko hayo kati ya kura 2,964 zilizopigwa.

China ilikuwa imeweka ukomo wa mihula miwili kwa nafasi ya urais tangu mwaka 1990 ambapo Xi Jinping alipaswa kukamilisha mihula yake mwaka 2023.

Ukomo huo uliwekwa kwa lengo la kukwepa uwepo wa kiongozi atakayekaa madarakani muda mrefu kama Mwenyekiti Mao Zedong.

Congress nchini China ndicho chombo chenye mamlaka ya juu zaidi ya kupitisha sheria na kupigia kura mapendekezo ya mabadiliko ya vifungu vya Katiba.

Kampuni yataka kumuuzia Beyonce jina la mwanaye, wavutana
Video: Sura mpya ya Dogo Janja yaibua hisia mpya