China imeonesha ndege yake mpya ya kivita yenye uwezo mkubwa wa kukwepa rada na kushambulia maeneo magumu kufikika.

Ndege hiyo iliyopewa jina la Wing Loong II imetengenezwa kwa teknlojia ambayo inaifanya kuwa ngumu kuonekana kwenye rada au vifaa vingine vya kunasa ndege.

Ina uwezo wa kubeba kilo 400 pamoja na kuunganishiwa aina mbalimbali za makombora yatakayoiwezesha kufanya mashambulizi, na itakuwa inaongozwa na rubani mmoja ambaye atakuwa ardhini akitumia rimoti.

Nchi hiyo imeionesha ndege hiyo kwenye kipande cha video, na imeelezwa kuwa ndege hiyo imekusudiwa kwa ajili ya soko lake la nje la silaha.

Aidha, hatua hiyo ya kuionesha ndege hiyo imekuwa wakati ambapo China iko katika mpango wa kuiuzia Pakistani ndege 48 zisizo na marubani zilizotengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu.

The Indian Express imeripoti kuwa ndege hiyo itakuwa na uwezo wa kusafiri angani kwa saa 20 bila kuongeza mafuta.

Msanifu mkuu wa ndege hiyo, Li Qidong amekaririwa na Xinhua akieleza kuwa ndege hiyo ya kivita ina uwezo wa kutua kwa dharura katika hali ambayo haikutarajiwa ikichagua yenyewe viwanja vya ndege vilivyo salama.

Mbunge mbaroni kwa tuhuma za kutaka kumuua Rais
Wanafunzi 20,000 elfu waacha shule