Serikali ya China imetangaza kufunga shughuli zote za kawaida kwenye mji wa Lanzhou wenye watu takriban milioni 4 na kuaamuru watu kutotoka nje isipokuwa kwa dharura ikiwa ni jitihada kudhibiti maambukizi ya Covid 19.

Vizuizi hivyo vinatolewa wakati China ikitoa taarifa ya visa 29 vipya vya maambukizi ya ndani ya Covid-19 vikiwemo sita katika mji wa Lanzhou, ambao ni mji mkuu wa jimbo la Kaskazini Magharibi la Gansu.

Huduma za Mabasi ya umma na magari ya kukodi tayari zimesimamishwa katika Mji huo, na vyombo vya habari vinasema mamlaka ya reli ya Lanzhou imesimamisha safari 70 za Treni, ikiwemo ya kwenda Beijing na Xi’an.

Mlipuko wa hivi karibuni unahusishwa na aina ya virusi inayosambaa kwa kasi ya Delta, inayofanya jumla ya visa 198 tangu Oktoba 17. na 38 ya visa hivyo vikibainika katika mji Lanzhou.

Urafiki bado kidogo uniponze
Simba SC vs Polisi Tanznaia