Baada ya takribani wiki sita za minong’ono kuwa huenda kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un aliitembelea China, nchi hiyo imethibitisha ziara hiyo na kuweka picha za viongozi wa nchi hizo wakiwa pamoja.

Picha zinazomuonesha Rais wa China, Xi Jinping na Kim Jong un zinaweka rekodi ya ziara ya kwanza ya kiongozi huyo wa Korea Kaskazini nje ya nchi tangu alipoingia madarakani mwaka 2011.

China ni mshirika mkuu wa kiuchumi wa Korea Kaskazini, hivyo iliaminika kuwa atafanya ziara hiyo wakati anajiandaa kukutana na rais wa Korea Kusini, Moon Jae-in pamoja na rais wa Marekani, Donald Trump.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa, Kim anatarajiwa kukutana na rais wa Korea Kusini Aprili kabla ya kukutana na rais Trump Mei mwaka huu.

 

Hatua hiyo ni ishara nzuri ya kumaliza mzozo wa muda mrefu kati ya Korea Kaskazini na nchi hizo, kufuatia majaribio ya makombora ya mabomu ya nyuklia.

Diamond afikia maridhiano na Serikali, 'maadili kwanza'
Jacqueline amwandikia ujumbe mzito mume wake, Reginald Mengi