Mamlaka nchini China imeamua kuwafungia ndani (lockdown) watu takribani milioni 1.2 wa Jiji la Yuzhou, baada ya kubaini kuwa watu watatu katika jiji hilo wamekutwa na Uviko-19, Januari 3, 2021.

Uamuzi huo ulifikiwa jana, China ikiwa kwenye jitihada za kuhakikisha hakuna mgonjwa wa Uviko – 19 wakati jiji la Beijing linaandaa michuano ya Olympics itakayoanza mwezi ujao.

Mamlaka ya Jimbo la Yuzhou, Henan imetangaza ‘lockdown’ ikiwataka wakaazi wa jiji hilo kubakia nyumbani.

Usafiri wa umma umezuiwa na magari hayaruhusiwi kuonekana barabarani isipokuwa magari ambayo yanahusika na mapambano dhidi ya uviko-19. Sehemu zote za burudani, maduka na maeneo mengine ya umma yamefungwa.

Mapema leo, China imeripoti visa vipya 175 vya uviko-19. Ingawa idadi hiyo inaonekana kuwa ndogo kwa kulinganisha na maeneo mengine duniani, idadi hiyo ni kubwa kuwahi kurekodiwa nchini humo kwa siku moja tangu Machi 2020.

Dkt. Mwigulu ataja zilipoenda fedha za tozo za miamala
Young Africans yaelekea Zanzibar