Aliyekuwa kocha wa timu ya Geita Gold Mine, Choke Abeid ameachiwa huru kuendelea na shughuli za soka baada ya awali kufungiwa kujihusisha na mchezo huo kutokana na tuhuma za kupanga matokeo.

Akizungumza juu ya uamuzi huo wa kumuachia Choke, Mwenyekiti wa Kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania, Rahim Shaban Zuberi amesema kuwa kocha huyo hakuwa na kosa lolote ambalo amelifanya baada ya kumshawishi kipa wa timu ya JKT Kanembwa arudi uwanjani kuendelea kudaka wakati timu hizo zilipokutana msimu wa 2015/16.

Ikumbukwe kuwa Choke akiwa Geita alikuwa ni msaidizi wa Seleman Matola ambaye ndiye aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, adhabu yake ilitolewa wakati wa utawala wa Jamal Malinzi ambaye kwa sasa anaelekea kumaliza muda wake na hayumo kwenye orodha ya wanaowania kutetea nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu wa TFF ujao.

“Kama kamati tumekaa na kuliangalia suala la kocha huyo na kubaini kuwa hakuwa na kosa lolote lile baada ya kumshawishi kipa wa wapinzani wao arudi uwanjani kuendelea kucheza, hivyo tunatangaza kwamba yuko huru kutoka kwenye kifungo cha maisha ambaycho alihukumiwa mwanzo.

“Lakini kamati pia ilipitia rufaa za watu wengine ambao walihukumiwa kutojihusisha na soka wakiwemo Yusuph Kitumbo, Fatch Rhemtullah na Thomas Mwita, hawa adhabu yao itaendelea kama ilivyo mwanzo,” alisema.

Wakati huo huo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza kumfutia kifungo cha kutojihusisha na masuala ya soka wakili Damas Ndumaro ambaye alifungiwa kwa muda wa miaka saba.

Maamuzi hayo yamechukuliwa na Kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya TFF chini ya mwenyekiti wake, Rahim Shaban Zuberi ambaye ndiye aliyetangaza maamuzi hayo kwenye ofisi za TFF zilizopo Karume jijini Dar es Salaam, leo Jumatano.

Hadi anafikia hatua ya kufunguliwa, Ndumbaro alikuwa ametumikia adhabu yake kwa muda wa miaka miwili na nusu.
Katika maelezo yake, Zuberi amesema Ndumbaro hakupata nafasi ya kujitetea na kuna badhi ya mambo hayakuzingatia usawa wakati akifungiwa.

Dkt. Mwakyembe na familia yake katika ibaada ya mazishi ya mke wake Linah
Waziri Mkuu Majaliwa na mkewe wakiweka shada