Chombo cha anga za juu cha China kinachojulikana kwa jina la Tiangong-1 ambacho kimekuwa kikitumiwa kama maabara kinatarajiwa kuanguka duniani mwishoni mwa wiki.

Chombo hicho kina urefu wa mita 10 na uzani wa zaidi ya tani 8 na ni kikubwa zaidi ya vyombo vyote vilivyoundwa na binadamu ambavyo vimewahi kuanguka kutoka anga za juu.

Aidha, China imesema kuwa imepoteza mawasiliano yote na chombo hicho jambo ambalo linamaanisha kuwa mwendo wake wakati kinadondoka kutoka anga za juu hauwezi kudhibitiwa.

Hata hivyo, wataalamu wamesema kuwa uwezekano wa vipande vya Tiangong ambavyo havitakuwa vimeteketea kabisa wakati vikifika ardhini kuanguka kwenye maeneo yenye watu wengi ni mdogo sana.

“Ukizingatia kwamba Tiangong-1 ina uzani wa juu sana, vipande vyao vimekazwa sana, kuliko ilivyo kwa vitu vingine ambavyo hurejea duniani kutoka anga za juu, kumekuwa na juhudi nyingi za kutumia mfumo wa rada kufuatilia mwendo wake na kukadiria ni wapi kitaanguka,” amesema Richard Crowther, mhandisi mkuu katika Shirika la Anga za Juu la Uingereza

 

Waasi wavamia nyumba ya Rais Kabila
Tiffany awatolea uvivu wanaohangaika kujua aliyemng’ata Beyonce usoni