Chombo cha Anga za juu cha China Tiangong-1 kimemeguka vipande na kuanguka maeneo ya bahari kusini mwa Pacific.

Tiangong-1 ilirushwa angani mwaka 2011 kufanyia majaribio ya teknolojia ya kuunganisha vyombo mbalimbali vya anga za juu na pia vyombo vya kuzunguka kwenye mzingo wa dunia.

Wataalamu wa anga za juu wa Marekani wamesema kuwa wametumia teknolojia ya kufuatilia mzingo wa dunia kuthibitisha kuingia ardhini kwa Tiangong-1

Hata hivyo, Shirika la Anga za Juu la Ulaya lilisema mapema kwamba uwezekano mkubwa ni kwamba chombo hicho cha Tiangong-1 kingeanguka baharini.

Erdogan, Netanyahu wazidi kushambuliana kuhusu Gaza
Kikosi cha Simba chaanza safari kuelekea Njombe