Katibu mkuu wa chama cha Mapinduzi – CCM, Daniel Chongolo amemuagiza Meneja wa Tarura Mkoa wa Iringa, Mhandisi Makoli Kisare kutengeneza barabarani ya kilomita moja ya kuelekea kituo cha afya Ifingo kata ya Kinyambo kuanzia kesho, ili kupunguza adha kwa wananchi wanaokwenda kupata huduma katika kituo hicho.

Chongolo ametoa agizo hilo Mei 27, 2023 baada ya kukagua kituo cha afya Ifingo ambapo wananchi wamelalamika kwa Katibu Mkuu changamoto ya barabara ya kuelekea katika kituo hicho, pamoja na kutokuwepo kwa daktari wa upasuaji.

Akitoa agizo kwa Meneja huyo wa Tarura, Chongolo amemtaka hadi kesho Mei 28, 2023 barabara hiyo ya kilomita moja iwe imeanza kutengenezwa ili kuwaondolea adha wananchi ya kuzunguka mwendo mrefu kufuata huduma za afya.

Katika hatua nyingine Chongolo amemuagiza Mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendegu kuhakikisha hadi kesho kituo hicho cha afya cha Ifingo pia kiwe kina daktari anayeweza kutoa matibabu ya upasuaji, ili wananchi wawe na uhakika wa matibabu wanapofika katika kituo hicho.

Chongolo yupo Mkoani Iringa kwa ziara ya siku 7 ya kukagua uhai wa chama na kukagua utekelezaji wa Ilani ya ccm ya mwaka 2020-2023 ambapo ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Sophia Mjema na Katibu wa Nec Oganaizesheni Issa Haji Gavu.

Wenye ulemavu wanatengwa, wanabaguliwa - Othman
Title: Meridianbet Yazindua Duka Jipya Ubungo-Kibangu