Chris Brown amepata hasira baada ya Marion “Suge” Knight ambaye alikuwa Boss na rafiki wa karibu wa 2 Pac kudaiwa kumfikisha mahakamani kwa kufuatia tukio la kupigwa risasi mwaka 2014.

Suge Knight ambaye alikuwa mwanzilishi waDeath Row Records, alipigwa risasi takribani 7 mwaka 2014 katika moja kati ya matukio aliyoyaandaa Chris Brown katika klabu ya usiku ya 1Oak iliyoko Hollywood, usiku wa kuamkia utoaji MTV VMA2014.

Kwa mujibu wa ABC, katika mashtaka yake, amedai kuwa Chris Brown alishindwa kuweka ulinzi imara hali iliyopelekea mtu mmoja kuweza kupenya na silaha na kumshambulia.

CNN imefanya mahojiano na mwakilishi wa Suge Knight ambaye ameeleza kuwa wao wanahitaji Chris Brown aweze kulipa fidia ya gharama zote za matibabu na mengine yatakayoamriwa na mahakama.

Breezy amechukizwa na hatua hiyo na kuamua kujibu kwa kejeli akitumia mfano mzito. Mwimbaji huyo ametumia mtandao wa Instagram kuweka habari ya kutengeneza yenye kichwa cha habari kinachoonesha kimeandikwa na mtandao maarufu wa ‘TMZ’ kuwa P Diddy (ambaye alikuwa hasimu wa 2 Pac)  anamshtaki Chris Brown kuhusu tukio la 2 Pac Shakur kupigwa risasi mwaka 1996.

Chris 2

Katika ‘post’ hiyo, mwimbaji huyo ameandika, “huu utakuwa upuuzi mwingine watakaosema baada ya huu. Angalia jinsi ilivyo rahisi kutengeneza upuuzi na ukaonekana kama uhalisia”.

Akamatwa kwa kuweka nyeti zake kwenye 'scanner' ya ukaguzi 'Supamaketi'
Uganda Kukomesha Mambukizi Mapya ya VVU kwa Watoto Wachanga 2017