Chris Brown ameshindwa kuvumilia tuhuma za wizi wa kofia zilizowasilishwa mahakamani na shabiki wake.

Shabiki huyo alieleza kuwa alimpa Chris Brown kofia yake kwa ajili ya kupata saini yake (autograph) lakini hakurudishiwa. Alieleza kuwa alipojaribu kuirejesha kofia yake, watu wa Breezy walimshambulia na kumpiga.

Kutokana na tukio hilo, shabiki huyo anadai kulipwa fidia ya $25 kwa ajli ya kofia yake, $225 kwa ajili ya tiketi yake na $2,500 kama fidia ya kuburuzwa na watoto.

Breezy ameamua kumjibu shabiki huyo kwa ku-comment kwenye ukurasa wa Instagram wa balleralert, akimtaka aache kumzushia na kwamba kama anahitaji kofia mpya aseme ampe kofia kali zaidi.

Comment

Audio: Raymond aeleza alivyoshiriki kuandika 'hits' za Diamond, Janjaro
Aitor Karanka Kutupa Ndoano Kwa Fernando Llorente