Wizkid Ayo wa Nigeria, bila shaka kwa sasa ndiye msanii wa Afrika anayepenya zaidi kwenye milango na masikio ya mastaa wa Marekani wanaompigia ‘salute’ kwa kazi zake.

Muziki wa Wizkid umeweza kumshawishi swahiba wake, Chris Brown kumpa shavu litakalompigisha hatua nzito kwenye muziki akipata mashabiki wapya barani Ulaya.

Kwa mara ya kwanza, Breezy amemuunga msanii wa Afrika anayefanya kazi zake akiwa Afrika kwenye ziara yake kubwa aliyoibatiza jina la ‘One Hell of a Nite Tour’, itakayozigusa nchi za Ujerumani, Denmark na Uholanzi.

Breezy amethibitisha shavu hilo kupitia Instagram akimpost Wizkid Ayo.

Wizkid  -Chris Tour

Kiongozi wa Upinzani ashambuliwa, uso wafurika misosi
Asimulia Maisha ya Kitwanga baada ya kutumbuliwa

Comments

comments