Mwanamuziki Chris Brown amelazimika kupiga simu na kutoa taarifa kwa jeshi la polisi huko California nchini Marekani, baada ya kubaini kuwa anawindwa na mwanamke mmoja aliyeonekana kunyemelea eneo la nyumba yake mara kwa mara.

Kwa mujibu wa TMZ na Idara ya Polisi ya Los Angeles, mwanamke huyo alikuwa akipita na kusimama mara kwa mara kwenye lango kuu la kuingilia kwenye makazi ya Chris Brown yaliyopo San Fernando Valley hadi kufikia hatua ya kumfanya msanii huyo kuhofia uwepo wa mwanamke huyo kiasi cha kuwaita polisi.

Taarifa zinasema kuwa wakati ambao maofisa wa polisi walifika katika eneo hilo, mwanamke huyo alidaiwa kutoka nje kabisa ya eneo hilo na inaelezwa kuwa simu aliyoipiga Brown kuwaita polisi ni simu ya tatu zikimuhusu mwanamke huyo mmoja ndani ya wiki chache zilizopita na kuonesha dalili za kuwa mwanamke huyo asiwe salama kwa Chrs brown.

Kwa mujubu na LAPD, mwanamke huyo ameonekana karibu na makazi ya Brown mara 10, ingawa haijulikani anataka nini kwa Brown au kwa nini anaendelea kuonekana mbele ya lango kuu la msanii huyo.

Kitendo cha Chris brown kupiga simu polisi ni kufuatia hofu yake juu ya masuala mbali mbali ya kisheri yaliyowahi kumkumba kutokana na wanawake.

Katika kipindi cha miaka iliyopita mara kadhaa yalimkuta matukio yaliyomfanya kuwa mjadala kote duniani licha ya kuwa mengine yalitokana na nia ovu na mipango mibaya ya kumchafua mwimbaji huyo.

Ikumbukwe Mnamo Machi, wakili anayemwakilisha mwanamke ambaye alidai kuwa Brown alimnyanyasa kingono na kumnywesha dawa za kulevya akiwa ndani ya boti iliyotiwa nanga nyumbani kwa Diddy mnamo Desemba 2020 na mwanamke huyo aliripotiwa kujiondoa katika kesi hiyo baada ya ujumbe wa maandishi wa mlalamishi kuvuja ukidhihirisha kuwa kesi ile ilikuwa ni mpango wa kumdhalilisha msanii huyo.

“Hakuna tena kuniburuta kwenye tope, NI WAZI WOTE MNAWEZA KUONA Sasa wacha tuone kama vyombo vya habari vitaweka nguvu zile zile walizokuwa nazo kujaribu kuniangamiza, katika kuendesha stori halisi,” aliandika Brown.

“Mimi na timu yangu tunachukua hatua za kisheria kuhusu hali hii. hupaswi kucheza na maisha ya watu hovyo.” aliandika Chris brown kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram akikemea vikali michezo inayofanywa kujaribu kumpaka matope.

Mitihani ya Taifa kusahihishwa kidijitali
Simba SC yaiweka kiporo Young Africans