Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Wales, Chris Coleman ametangaza marufuku kwa wachezaji wake kusafiri na marafiki zao wa kike pamoja na wake zao, wakati wa fainali za mataifa ya barani Ulaya (Euro 2016) zitakazofanyika nchini Ufaransa baadae mwaka huu.

Coleman, ametangaza marufuku hiyo, akiwa mbele ya waandishi wa habari, ambapo lengo kubwa la kufanya hivyo ni kutaka kuwaona wachezaji atakaowaita kwa ajili ya fainali hizo, kugeuzia mawazo yao katika michezo mitatu ya hatua ya makundi.

Amesema jukumu kubwa litakalowapelekea nchini Ufaransa, litakua ni kushindana, na si kwenda kufanya matembezi ya kutalii ama kupumzika katika fukwe za bahari.

Akitolea mfano ambao umempa hofu ya kuliruhusu jambo hilo, Coleman ambaye aliwahi kufanya kazi katika baadhi ya klabu za soka nchini England, amesema wachezaji wa taifa hilo walishindwa kufika mbali katika fainali za kombe la dunia za mwaka 2006, kutokana na kocha kwa wakati huo Sven Goran Erickson, kuruhusu jambo hilo kuchukau nafasi kwenye kambi.

“Tutakabiliwa na michezo mitatu ya hatua ya makundi, na hatuna budi kupambana ili tuweze kufanikisha harakati za kushinda na kusonga mbele, hivyo kila mmoja wetu atatakiwa mawazo na akili yake katika mtihani huo,” alisema Coleman, ambaye ataweka kambi katika hoteli ya Dinard iliopo kwenye ufukwe wa Brittany nchini Ufaransa wakati wa fainali za Euro 2016.

“Michezo hiyo mitatu itatulazimu kuicheza ndani ya siku 10, na hatutokua na muda wa kupoteza, zaidi ya kujiandaa, kusafiri pamoja na kucheza” alisisitiza kocha huyo raia wa Wales.

Wales imepangwa kundi moja dhidi ya Slovakia, England pamoja na Urusi na haijawahi kushiriki fainali kubwa za soka tangu mwaka 1958, walipocheza kwa mara ya kwanza fainali za kombe la dunia.

Mmiliki Wa Newcastle Utd Atoboa Siri Ya Kumuajiri Benitez
Abdi Banda Amvuruga Kocha Wa Simba Jackson Mayanja