Kiungo wa mabingwa wa soka barani Afrika, timu ya taifa ya Cameroon Christian Bassogog amejiunga na klabu ya Henan Jianye inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini China, akitokea Denmark alipokua akiitumikia klabu ya AaB Fodbold.

Mapema mwezi huu, kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21, alitajwa kuwa mchezaji bora wa fainali za mataifa ya Afrika zilizofanyika nchini Gabon (AFCON 2017).

Klabu ya AaB imethibitisha kufanya biashara na Henan Jianye FC na kuweka taarifa hizo katika tovuti yake.

Bassogog aliambia tovuti ya klabu ya AaB, ilikua ni vigumu kwake kukataa ofa ya kuelekea nchini China tangu aliposikia Henan Jianye wapo tayari kumuhamisha.

Uchunguzi uliofanywa na shirika la utangazi la Uingereza BBC umebaini kuwa, klabu ya Henan Jianye imemsajili kiungo huyo kwa ada ya Pauni milioni 8.7.

Bassogog aliitumikia timu yake ya taifa katika michezo yote ya AFCON 2017, kwa kujumuishwa kwenye kikosi cha kwanza na aliifungia Cameroon bao muhimu wakati wa mchezo wa nusu fainali dhidi ya Ghana, waliokubali kufungwa mabao mawili kwa sifuri.

Wazalishaji viroba wapewa masharti sita.
Mark Clattenburg Kusubiri Mwishoni Mwa Msimu