Wasanii Christan Bela na Walid watatoa burudani ya kipekee katika Tamasha la Seafood Gala linalotarajiwa kufanyika Siku ya Sikukuu ya Eid mossi.

Tamasha hilo litakalofanyika katika fukwe za ‘ESCAPE ONE’ Mikocheni kuanzia saa nane mchana litakuwa la aina yake ambapo vyakula mbali mbali vya baharini kama Pweza, Supu ya Pweza, Ulojo, Kacholi na Samaki vitakuwa vikipatikana.

Watakao hudhuria katika tamasha hilo watapata burudani mbalimbali ambapo licha ya vyakula na Show kali ya Christian Bella na msanii Walid anayetamba na ngoma yake mpya inayoitwa ‘Namna Gani’ akiwa amemshirikisha Patoranking kutoka Nigeria, wataweza kushuhudia live michuano ya kombe la Dunia.

Viingilio katika Tamasha hilo vitakuwa ni Shilingi 10,000/= kwa wakubwa na watoto Shiling 5,000/=.

UDSM yatoa ratiba ya kuaga miili ya wanafunzi waliofariki kwa ajali
Huu ndio ukweli kuhusu jumbe za uhamasishaji

Comments

comments