Mshambuliaji mpya wa klabu ya Crystal Palace Christian Benteke, amefunguka kwa mara ya kwanza tangu alipokamilisha azma ya kuondoka mjini Liverpool alipokua akiitumikia klabu nguli ya Anfield Liverpool FC.

Benteke ambeye alishindwa kumshawishi meneja wa Liverpool Jurgen Klopp ili aweze kuwa sehemu ya mipango ya kucheza katika kikosi cha kwanza, amesema alikua na wakati mgumu wa kukamilisha mpango huo.

Benteke amesema alijitahidi kadri awezavyo ili kumshawishi meneja huyo kutoka nchini Ujerumani, lakini ilikua ngumu kumuelewa na wakati mwingine alikaribia kukata tamaa.

Amesema pamoja na kukabiliwa na changamoto hiyo, bado alijipa matumaini na kuamini kuna nafasi ya kuendelea kucheza soka itajitokeza mbele ya safari ya maisha yake alipokua huko Anfiled, na siku kadhaa baadae alifarijika pale aliposikia atasajiliwa na Crystal Palace.

Mshambuliaji huyo kutoka nchini Ubelgiji ameahidi kupambana katika klabu hiyo mpya yenye maskani yake makuu huko Selhurst Park jijini London ili kumshawishi bosi wake mpya Alan Pardew.

Tayari ameshacheza mchezo mmoja tangu aliposajiliwa na Crystal Palace, lakini hakubahatika kuonyesha cheche za kufunga bao.

Benteke mwenye umri wa miaka 25, aliitumikia Liverpool katika michezo 42 tangu alipojiunga nayo akitokea Aston Villa mwanzoni mwa msimu wa 2015/16, na wakati wa utawala wa meneja Brendan Rodgers alionekana kuwa tegemeo katika safu ya ushambuliaji.

Brendan Rodgers alimsajili mshambuliaji huyo kwa dau la Pauni milioni 32, na kila shabiki anaefuatilia soka la nchini England aliamini Benteke angekua mshambuliaji bora chini ya kivuli cha Liverpool, lakini mambo yalimbadilikia na kujikuta akiishia benchi.

Serikali yamjibu Kitwanga, yatetea ununuzi wa ndege za Bomberdier Q400
FA Wamtega Sergio Aguero