Ikiwa leo ni tarehe ya mfanano wa siku aliyozaliwa msanii maarufu, Mrisho Mpoto, ameweka wazi jinsi ambavyo baba yake alibarikiwa kupata idadi kubwa ya watoto na yeye akiwa ‘Mziwanda’.

Mpoto ameeleza kuwa yeye ni mtoto wa mwisho kati ya watoto 36 wa baba yake ambaye alikuwa na wake 12.

Akizungumza kupitia Sun Rise ya 100.5 Times FM, Mpoto ameeleza kuwa mama yake alikuwa mwanamke wa 12 kwa baba yake na alijaliwa kuzaa watoto 12. Hii ina maana kuwa kwenye tumbo la mama yake yeye (Mpoto) ni mtoto wa 12 aliyefunga idadi ya watoto wa mzee Mrisho.

“Wanawake walikuwa 12, mama yangu alipata watoto 12, wanawake wengine walikuwa na watoto watano, mwingine wanane n.k…lakini wengine hawakuzaa,” alisema Mpoto.

Mpoto ni mmoja kati ya wasanii wenye historia ya kuvutia ya makuzi yake yaliyompelekea kuwa na uwezo mkubwa wa kukariri masimulizi ya vitabu mbalimbali na kuyasimulia kwa mtindo wa aina yake, hali iliyompelekea pia kuwa na uwezo mkubwa wa kuandika mashairi na kughani.

Dar24 inamtakiwa Mpoto heri ya siku yake ya kuzaliwa.

Jackson Martinez Kurejeshwa Ulaya
George Lwandamina Apokelewa Kwa Kichapo

Comments

comments