Kampuni ya Korea Kusini ya LG Electronics Inc imekuja na toleo jipya la TV yenye kioo chembamba aina LED ambayo inaweza kufukuza mbu pale inapowashwa.

LG wametumia teknolojia kuondoa kero ya mdudu mbu kwa watazamaji wanaotumia kifaa hicho, ambayo itakuwa ikitoa mawimbi ya sauti (ultrasonic wave) kupitia spika zake na kama mtumiaji atachagua kufukuza mbu, spika hizo zitatoa mawimbi ya sauti (sio sauti kubwa ni mawimbi ya sauti yenye frequency kubwa) yatakayofukuza mbu.

Kwa lugha ya kitaalam, spika hizo zitatoa mawimbi kwenye frequency ya zaidi ya ukubwa wa 30kHz, mawimbi ambayo binadamu hawezi kuyasikia na yasiyo na madhara kwa binadamu.

Kumbuka kuwa binadamu anaweza kusikia sauti yenye mawimbi kati ya 20Hz hadi 20kHz. Hivyo mawimbi ya 30KHz yatakuwa kwa ajili ya kuwatimua mbu pekee.

Hivyo kutakuwa na njia nyingine ya spika itakayotoa mawimbi yenye usikivu kwa binadamu.

 

Ali Kiba ataka Wizkid ‘aachwe’
Mahakama yampa dhamana Lema, Hatua ya Serikali yamrejesha

Comments

comments