Dar es salaam kumekuwa na utapeli mkubwa unaofanyika kwa njia ya simu ambapo watu wasiojulikana hutuma ujumbe kwa watu mbalimbali wakijifanya walikuwa na miadi ya kutumiwa hela hivyo kutoa maelekezo juu ya kutumiwa pesa hizo kupitia namba fulani wakijifanya simu zao zimezima hivyo pesa hiyo itumwe kwa wakala.

Wengi wamekwishalizwa na utapeli huo wa kutumia mbinu hiyo na mbinu nyingine nyingi.

Unakuta ujumbe unaingia kwenye simu ukisomeka hivi.

”Kutoka namba +255 621 314 714, ile hela itume kwenye namba hii 0767 432 449 sm yangu inasumbua sana nipo kwa wakala hapa fanya haraka.

Kama kweli ulikuwa unadeni linalokusumbua au mtu anaokusumbua juu ya kulipa deni lake mara ukutanapo na ujumbe huu unaweza kujikuta kweli ukituma hizo fedha kumbe unatuma kwa mtu ambaye sio sahihi, au kama ulikubaliana na mtu unamtumia hela gafla ukapata huo ujumbe unaweza kujikuta kweli ukiingia mkengeni.

Wengine hufanya utapeli kwa njia ya kujifanya mganga wa kienyeji  unaweza kukutana na ujumbe unaosomeka hivi.

”Mjukuu wangu ndagu niliyokukabizi hiyo uwe makini na pesa hizo zinakuja usiogope ndio mafanikio yako si nilikwambia utafanikiwa usimwambie na mwingine nipigie ili nikuelekeze”.

Lakini pia hii michezo ya bahati na sibu inayofanyika imezua utapeli wa aina nyingi sana katika Jamii kupitia mtandao wa simu ambapo mtu anaweza kukupigia simu na kudai umeshinda kiasi fulani cha pesa, kisha huuliza kwa kiasi iko cha pesa akaunti yako itakuwa na kiasi gani kosa kubwa linalofanywa na watu wengi bila kujua ni kutaja kiasi sahihi cha pesa aliyonayo kwenye simu na ndipo watu wengi huibiwa kwa kukombewa fedha zote alizonazo kwenye akaunti ya simu yake.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA imesema kisheria haina jukumu la kudhibiti uhalifu huo ila itajitahidi kushirikiana na jeshi la polisi kitengo cha makosa ya mtandaoni ikiwezekana kutumia teknolojia kupambana na wahalifu hao.

Taasisi nyingine za Mawasiliano kama Tigo imetoa wito kwa wateja wote kuwa makini sana na matumizi ya simu ili kuepusha uhalifu huo unaofanywa na wajanja wa mjini.

Heche aitaka serikali kuacha kuwatesa wafugaji
R. Kelly abanwa tena kwa unyanyasaji wa kingono

Comments

comments