Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewaagiza waajiri wasiopeleka au kuchelewesha michango ya wanachama kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii nchini wachukuliwe hatua za kisheria ili kukomesha tabia hiyo.

Ameyasema hayo  Jijini Mwanza wakati anafungua semina ya maisha baada ya kustaafu,fursa ya mafao,uwekezaji iliyoandaliwa na Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF)kwa ajili ya wastaafu watarajiwa 450 kutoka wilaya zote za mkoa wa Mwanza..

Aidha, amewahakikishia Wakurugenzi wa mifuko hiyo kuwa Serikali inashughulikia madeni yote na baada ya kukamilika kwa zoezi la uhakiki wa madeni hayo basi malipo yatafanyika haraka iwezekanavyo.

 

“Wazee ni rasilimali na hazina kubwa kwa taifa kama waswahili wasemavyo panapo wazee hapaharibiki jambo hivyo basi ni matumaini yangu kuwa mfuko wa PSPF mtaendelea kufanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu kuhakikisha kuwa hazina hii ya wazee wetu wanapata haki zao kwa mujihu wa sheria za nchi pale wanapohitaji huduma toka kwenu,”amesema Samia Suluhu.

 

 

Real Madrid watwaa ubingwa UEFA
Beckham awachanganya wazazi kwa busu alilompa mwanae wa kike akiwa Afrika