Rais wa Jamhuri ya Muungano Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania inatarajia kujenga chuo cha TEHAMA kwa ajili ya kuwasaidia vijana kujikamua kiuchumi kutokana na swala la ukosefu wa ajira.

Rais Samia ameyasema hayo leo oktoba 17 katika hotuba yake kwa wananchi wa Arusha katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid akiendelea na Ziara ya kutembelea na kuzindua miradi ya maendeleo mkoani Arusha.

“Najua na ninatambua ugumu mnaoupitia vijana kwa kukosa ajira, kwa bahati nzuri nimepata mdau ambae tutashirkiana kujenga chuo kikubwa sana cha TEHAMA ambapo vijana tutawafunza ili mpate ubunifu na kuweza kujiajiri” amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema anaendelea kutafuta fedha ili kujenga maeneo ambayo yatakua na huduma zote ambayo vijana wataweza kukaa na kufanya shughuli zao za kujitafutia kipato.

Asilimia 65 ya watu wa Tanzania ni vijana, najua wengi wenu hamna ajira, mmemaliza shule na hamna ajira mama yenu silali naangalia wapi nitanasa fedha mtapata ajira nahangaika kutafuta fehda kwa ajili yenu na Mungu Inshaallah anisaidie nizipate ili kutimiza ndoto hiyo” ameongeza Rais Samia.

Rais Samia amesema Serikali kupitia wasaidizi wake inaendelea kuwaangalia vijana wote ikiwa ni pamoja na wale wanaoingia katika elimu ya juu kwa kupata mikopo na kuongeza idadi ya vyuo vya Veta kwa kuwa vijana ndio Injini ya maendeleo.

Katika Hatua nyingine Rais Samia amekabidhi fedha kwa vikundi vya wanawake vijana na walemavu kiasi cha shilingi bilioni 1.3 kwa ajili ya kuwainua makundi hayo kiuchumi katika kazi zao za viwanda vidogo ili kuleta maendeleo na ajira.

Awali Rais Samia amewataka wananchi na viongozi wa maeneo tofauti ambao wanataka maeneo yao yapandishwe hadhi ya kuwa Wilaya au Mikoa wawe na uvumilivu kwa kuwa kwa sasa Serikali inaangalia namna ya kupata fedha kwa ajili ya kuwakwamua wananchi kiuchumi baada ya Janga la UVIKO-19.

Wanufaika wa HESLB waula
Kutumia picha za kughushi ni kosa kisheria:Serikali