Mkurugenzi wa mafunzo ya ufugaji nchi wa kisasa katika kituo cha Tanzania Bee Keeping Village cha kisaki kiichopo Halmashauri ya Manispaa ya Singida, Philemon Kiem alibainisha mpango wa kujenga chuo kikuu cha ufugaji nyuki.

Chuo hicho kitakuwa ni muendelezo wa kituo cha mafunzo ya nyuki ambacho kitaboreshwa miundombinu iliyopo kama ujenzi wa nyumba sita zenye ghorofa sita kilamoja na ujenzi huo unatarajiwa kushirikisha Serikali na wadau wake wa nje na ndani.

Mipango huyo imebainishwa wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya ufugaji wa kisasa wa nyuki mkoani Singida ambapo hadi sasa jumla ya watu 778 kutoka ndani na nje ya mkoa wa Singida wamepata mafunzo ambayo yalitolewa kati ya mwaka 2014 na 2018.

Mafunzo ya ufugaji bora wa nyuki huwajengea washiriki uwezo wa kutumia rasilimali ya nyuki vizuri katika biashara za uuzaji wa asali na mazao mengine ya nyuki na kutunza mazingira kwenye maeneo walipotoka na wengiwao wakiwa vijana.

Ubakaji watoto watikisa Kibiti
Sahle-Work Zewde achaguliwa kuwa rais wa Ethiopia

Comments

comments