Shirika la Kijasusi Nchini Marekani CIA limeingiwa na wasiwasi Juu ya Mipango ya Rais Mteule wa Marekani Donald Trump, ya kusitisha makubaliano ya mpango wa nyuklia na Iran na kusema kuwa kufanya hivyo itahatarisha Usalama wa Taifa hilo kubwa lenye nguvu duniani.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Shirika hilo, John Brennan alipokuwa akifanya mahojiano na vyombo vya habari nchini humo, ambapo amemshauri Rais huyo mpya kuwa na tahadhari kubwa kuhusu ahadi na matamko yake ambayo amekuwa akiyatoa kulingana na mustakabari wa sera zake.

Aidha, Brennan amesema ahadi za Trump kuhusu kuwa na mahusiano ya karibu na Urus, ni hatari zaidi kwani nchi hiyo inahusika na upotevu wa amani nchini Syria                                                                                                                                                                                               .

Brennan alitaja mambo machache ambapo alisema kuwa utawala mpya unatakiwa kuyazingatia kwa busara na hekima, ikiwemo lugha inayotumiwa kuhusu Ugaidi, Uhusiano na Urusi, mpango wa kinyuklia wa Iran na siri za Shirika hilo hutekelezwa

Lukuvi ayageukia mabaraza ya ardhi, aonya kukithiri kwa rushwa
Obama afunguka kuhusu mpango wa Mkewe kugombea Urais Marekani