Bao la Kiungo kutoka nchini Zambia na Klabu ya Simba SC Clatous Chotta Chama dhidi ya Horoya AC, limechaguliwa kuwa bao Bora la Ligi ya Mabingwa Barani Afrika Mzunguuko watano uliofikia tamati mwishoni mwa juma lililopita.

Bao la kwanza la Simba SC katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Jumamosi (Machi 18) lilifungwa na kiungo huyo kwa mkwaju wa adhabu ndogo nje ya lango la Horoya AC, ndilo limeibuka kidedea na kuchaguliwa kuwa Bao Bora la Wiki.

CAF imethibitisha kuchaguliwa kwa Bao hilo la Chama kupitia vyanzo vya Habari vya Shirikisho hilo la soka Barani Afrika.

Taarifa iliyochapishwa na CAF iliyoenda sambamba na Video ya Bao hilo imeeleza: Bao la Clatous Chama dhidi ya Horaya AC limechaguliwa kuwa Bao Bora la Wiki katika mzunguuko wa 5

Baada ya taarifa hizo Simba SC kupitia kurasa zake za Mitandao ya Kijamii nayo iliandika: Goli la Clatous Chama ambalo alifunga kwa mpira wa faulo dhidi ya Horoya AC limechaguliwa kuwa Goli Bora la Wiki la Ligi ya Mabingwa Afrika kwa michezo ya mzunguko wa tano. #GoalOfTheWeek

Endelea kumpigia kura Chama au Kanoute ambao wanawania kuwa Mchezaji Bora wa Wiki wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kura zinapigwa kwenye ukurasa wa Twitter wa CAF unaohusika na mashindano ya vilabu.

Dkt. Mwanga: FADev, Serikali kuendeleza wachimbaji wadogo
Wawekezaji 23 waonesha nia Kongani ya kisasa Viwanda