Beki wa klabu bingwa Tanzania bara Young Africans, Vincent Bossou ameitwa kwenye kikosi cha awali cha timu ya Taifa ya Togo kitachoshiriki Fainali za Kombe la Mataifa Afrika mwezi ujao nchini Gabon.

Kocha mkuu Claude Le Roy pia ameendelea kumuamini mshambuliaji Emmanuel Adebayor licha ya kutokuwa na timu tangu aachane na Crystal Palace mwishoni mwa msimu uliopita.

Bossou anakuwa mchezaji wa tatu anayecheza Ligi Kuu Tanzania Bara kujumuishwa katika kikosi cha awali cha AFCON baada ya beki wa Simba, Juuko Murshid kuteuliwa katika kikosi cha Uganda na Bruce Kangwa wa Azam kujumuishwa katika kikosi cha Zimbabwe.

Kikosi kamili cha awali;

Walinda Milango: Kossi Agassa (Huru ), Baba Tchagouni (FC Marmande, Ufaransa), Cédric Mensah (Le Mans, Ufaransa)

Walinzi: Serge Akakpo (Trabzonspor, Uturuki), Sadate Ouro-Akoriko (Al Khaleej, Saudia Arabia), Djene Dakonam (Saint-Trond, Ubelgiji), Gafar Mamah (Dacia, Moldavie), Maklibè Kouloun (Dyto, Togo), Hakim Ouro-Sama (AS Togo Port), Vincent Bossou (Young Africans,Tanzania), Joseph Douhadji (Rivers United, Nigeria)

Viungo: Alaixys Romao (Olympiacos, Ugiriki), Matthieu Dossevi (Standard Liège, Ubelgiji), Floyd Ayité (Fulham, Uingereza), Henritsè Eninful (Doxa, Ujerumani ), Lalawele Atakora (Helsingborgs, Sweden), Prince Segbefia (Goztepe, Uturuki), Ihlas Bebou (Fortuna Dusseldorf, Allemagne), Franco Atchou (Dyto, Togo), Victor Nukafu (Entente II, Togo), Serge Gakpe (Genoa, Italia)

Washambuliaji:  Emmanuel Adebayor (Huru), Fo Doh Laba (Berkane, Morocco), Razak Boukari (Chateauroux, Ufaransa).

Video: Lema augua ghafla selo, Mauaji yaliyotikisa 2016...
Rais Wa PSG Haambiwi, Hasikii Kuhusu Arsene Wenger