Meneja wa klabu bingwa nchini England Leicester City Claudio Ranieri, amewasihi mashabiki wa The Foxes kumpokea kwa mikono miwili kiungo kutoka nchini Ufaransa N’Golo Kante, ambaye hii leo atarejea klabuni hapo akiwa na kikosi cha Chelsea.

Ranieri, amewasilisha ombo hilo kwa mashabiki, kufutia kikosi cha Chelsea kutarajia kucheza mchezo wa kombe la ligi (EFL) dhidi ya Leicester City katika uwanja wa King Power.

Kante, aliondoka klabuni hapo wakati wa usajili wa majira ya kiangazi na kujiunga na klabu ya Chelsea, jambo ambalo linachukuliwa na mashabiki kama aliisailiti Leicester City ambayo bado ilikua inamuhitaji katika kipindi hiki cha kutetea taji lao la PL.

“Ninafarijia kuona Kante anarejea tena hapa na nitampokea kwa furaha na bashasha kutokana na uhusiano wetu kuwa mzuri tangu nilipomsajili mwaka 2015 akitokea Caen.

“Ninataka kuona hata kwa mashabiki inakua hivyo, kwa sababu Kente bado ni sehemu ya familia yetu, ambae alionyesha kujituma na kupata mafanikio ya kutwaa ubingwa wa ligi msimu uliopita.”

“Mashabiki wanapaswa kufahamu kwamba, soka ni mchezo ambao una changamoto zake na wakati mwingine inakua ngumu kuamini kama mtu anaweza kukuacha katika kipindi unachomuhitaji, lakini bado ninasisitiza Kante ni mwenzetu na tunapaswa kumuheshimu kwa kiasi kikubwa.” Alisema Ranieli

Kante alikua mchezaji pekee aliyeamua kuondoka wakati wa majira ya kiangazi huku wachezaji wenzake waliochangia mafanikio ya kutwaa ubingwa wa England msimu wa 2015/16 Jamie Vardy na Riyad Mahrez, wakikubali kusaini mikataba mipya.

Klabu ya Arsenal ilionyesha ni ya kutaka kuwasajili Jamie Vardy na Riyad Mahrez lakini bado msimamo wao ulidhihirisha mapenzi na Leicester City.

Mario Balotelli Apigiwa Chepuo La Kurudi England
Wenger: Nilishangaa Kuona Bendtner Amesaini Nottingham Forest