Meneja wa vinara wa msimamo wa ligi kuu ya soka nchini England Leicester City, Claudio Ranieri amesema haoni pa kwenda kufanya kazi yake kwa sasa zaidi ya kumalizia ujuzi wa ukufunzi akiwa King Power Stadium.

Ranieri ambaye ameonyesha maajabu ya kukiunda kikosi cha The Foxes msimu huu na kukiwezesha kuwa katika mustakabili wa kutwaa ubingwa wa nchini England, amesisitiza jambo hilo baada ya kuulizwa na waandishi wa habari juu ya matarajio yake ya baadae.

Ranieri amesema haoni sehemu nyingine ya kufanya kazi kwa sasa, hasa ikizingatiwa umri wake wa miaka 64 haumruhusu kuhangaika huku na kule kusaka ajira, na badala yake anamshukuru mwenyezi mungu kwa kumuwezesha kupata mahala pa kutulia.

Hata hivyo, inaelezwa kwamba meneja huyo kutoka nchini Italia, anaandalia mkataba wa muda mrefu na uongozi wa klabu ya Leicester City kufuatia mambo mazuri aliyoyaonyesha tangu alipowasili mwaoznoni mwa msimu huu.

“Kazi ya kukinoa kikosi cha Leicester City itakua ya mwisho kwangu, na ninaamini nitakua hapa kwa muda mrefu zaidi tofauti na ilivyokua katika klabu kadhaa nilizowahi kuzitumikia kama meneja.

“Ninafurahia hali na mazingira ya klabu hii, na ninaamini mnayoyaona kwa msimu huu, nitajitahidi kuyaboresha zaidi ili kuleta chachu katika kazi yangu na kwa klabu pia.” Alisema Ranieri

Ranieri aliwahi kufanya kazi na klabu kadhaa za barani Ulaya ikiwemo Chelsea ya jijini London kuanzia mwaka 2000–2004, Lametini (1986–1987), Puteolana (1987–1988), 1988–1991), Napoli (1991–1993) na Fiorentina (1993–1997),

Nyingine ni Cagliari (Valencia (1997–1999) na (2004–2005), Atlético Madrid (1999–2000), Parma (2007), Juventus (2007–2009), Roma (2009–2011), Inter Milan (2011–2012) na AS Monaco (2012–2014)

Mbali na kufanya kazi na klabu hizo za mataifa mbalimbali ya barani Ulaya, Ranieri amewahi kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Ugiriki lakini alidumu na kazi hiyo kwa mwaka mmoja (2014).

Ommy Dimpoz ahamia kwenye kilimo
Lupita Nyong’o adai hana TV nyumbani kwake, awataja wanaompa habari