Taarifa za usajili wa kiungo kutoka nchini Algeria na klabu ya Leicester City Riyad Mahrez, zimeonekana kumchoshwa meneja wa klabu hiyo inayoshikilia taji la England, Claudio Ranieri.

Ranieri alionyesha kuchoshwa na taarifa za usajili wa kiungo huyo anayehusishwa na mipango ya kusajiliwa na klabu ya Arsenal, alipozungumza na waandishi wa habari mara baada ya mchezo wa jana, ambao ulishuhudia Leicester City akichabangwa mabao manne na mabingwa wa soka nchini Ufaransa PSG.

Ranieri aliulizwa na mmoja wa waandishi wa habari kuhusu usajili wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25, na alijibu kwa ukali swali hilo, kwa kusema amechoshwa na taarifa za kuondoka ama kubali kwa Mahrez, kikosini mwake.

“Labla Riyad atakua na majibu sahihi, lakini niaamini hata yeye ameshachoshwa na taarifa hizi ambazo kila siku zimekua zikizungumzwa na kuandikwa katika vyombo vya habari,” Alisema Ranieri

“Jambo kubwa ambalo ningependa kuzungumza nanyi ni kuhusu mwenendo wa kikosi changu ambacho kwa sasa kinajiandaa na msimu mpya wa ligi, lakini sio masuala ya usajili ambayo hayana uzito mkubwa kwangu kwa sasa. ” Alisisitiza babu huyo kutoka nchini Italia

Tayari Leicester City, wameshakubali kumuachia kiungo kutoka nchini Ufaransa N’Golo Kante ambaye amesajiliwa na Chelsea kwa ada ya Pauni milioni 32.

Senol Gunes Kukwamisha Usajili Wa Mario Balotelli
Coke Aondoka Sevilla CF