Meneja wa vinara wa ligi kuu ya soka nchini England, Leicester City Claudio Ranieri hatokua sehemu ya watakaoshuhudia mchezo wa hii leo wa ligi ya nchini humo kati ya Tottenham Hostpurs dhidi ya Chelsea.

Mchezo huo ambao huenda ukaamua hatma ya Leicester City kutwaa ubingwa msimu huu ama kuendelea kusubiri kutokana na sare ya bao moja kwa moja iliyopatikana jana kwenye uwanja wa Old Trafford, ulitegemewa huenda utafuatiliwa kwa ukaribu na meneja huyo.

Ranieri amethibitisha kwamba usiku wa hii leo anatarajia kuelekea nchini Italia kwa ajili ya kujumuika na wanafamilia wengine katika sherehe ya mama yake mzazi ambaye anatamiza umri wa miaka 96.

Ranieri amesema anajua hatua hiyo itamnyima nafasi ya kuwa shuhuda wa mpambano huo muhimu katika historia ya maisha yake, na huenda akawa mtu wa mwisho kufahamu matokeo ambayo yatakua chagizo la kufahamu nini mustakabali wa kikosi chake wa kutangaza ubingwa kabla ya mchezo wa mwisho kuchezwa.

Kikosi cha meneja huyo kutoka nchini Italia, kilitarajiwa huenda kingetangaza ubingwa katika uwanja wa Old Trafford hapo jana endapo kingeibuka na ushindi, lakini sare ya bao moja kwa moja dhidi ya Man Utd iliwanyima nafasi ya kushangilia wakiwa ugenini.

Endapo itatokea Spurs anapoteza mchezo wa hii leo mbele ya Chelsea, Leicester City watatangazwa kuwa mabingwa rasmi kutokana na pengo la point nane ambalo litakuwepo.

Baada ya mtokeo ya mchezo wa jana kati ya Leicester City dhidi ya Man Utd, vinara hao wa ligi walifikisha point 77.

Audio: Sikiliza ‘vutankuvute’ kati ya 'trafiki' na Mke wa Waziri iliyomfikia Rais Magufuli
CAG, Msajili wa Hazina wakinzana kuhusu Umiliki wa PRIDE