Kamati ya utendaji ya Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) imemuangua Mwenyekiti wa Bodi ya ligi (TPLB) Clement Sanga kutokana na kukosa vigezo.

Maamuzi hayo yametokana na klabu ya Yanga kupeleka barua TFF kuwa Mwenyekiti wao Yusuf Manji aliyekuwa amejiuzulu amerejea katika nafasi yake hivyo Sanga kukosa vigezo.

Kwa mujibu ya kanuni ya Bodi ya ligi Mwenyekiti wake anapaswa kuwa Mwenyekiti wa klabu kwahiyo baada ya Manji kurejea katika nafasi hiyo Sanga amekosa vigezo kwakua amekuwa Makamu.

Rais wa TFF, Wallace Karia amewaambia waandishi wa habari kuwa wamewasiliana na Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi juu ya hilo na ataandaa uchaguzi mdogo kwa ajili ya kuziba nafasi hiyo.

“Kikao cha kamati ya utendaji kimekutana na leo na moja ya maamuzi yaliyofanyika ni kumtoa Clement Sanga kuwa Mwenyekiti wa bodi ya ligi kwakua amepoteza vigezo kwakua Manji amerejea kwenye nafasi yake.

“Tumepokea taarifa kutoka kwa Katibu mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa kuwa mkutano mkuu umeridhia Manji kurejea katika nafasi yake hivyo Kamati imekubalina kumuondoa,” alisema Karia.

Ruhsa Rabiot kuondoka PSG, FC Barcelona wahaha
Achraf Hakimi atua Borussia Dortmund