Aliyekuwa mgombea wa kiti cha urais wa Marekani kwa tiketi ya Chama cha Democratic Hillary Clinton, amesema kuwa kushindwa kwake  katika uchaguzi uliopita, kulichangiwa na Mkurugenzi wa shirika la kijasusi la Marekani FBI, James Comey kutangaza uchunguzi  wa sakata la barua pepe dhidi yake muda mfupi kabla ya uchaguzi.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wafadhili wa chama chake kuwa hatua ya Comey ilisambaratisha kampeni yake, licha ya uchunguzi huo kutompata na hatia.

Profesa ala wadudu kutimiza ahadi aliyoitoa ‘kama trump akishinda Urais’
Utafiti: Wananchi vijijini washusha alama kwa utendaji wa Serikali kuliko wa mijini