Vituo vya Clouds FM  na TV vimerejea hewani baada ya kukamilisha kifungo cha siku saba kwa kosa la kuvunja sheria ya mawasiliano.

Siku ya alhamisi Agost 27 ,Mamalaka ya mawasiliano (TCRA) ilitangaza kuvifungia kwa siku saba  vyombo hivyo vya habari .

TCRA ilisema kuwa  imevifungia vituo hivyo  kwa kosa la kutangaza takwimu ambazo hazikuwa zimethibitishwa na tume ya taifa ya uchaguzi (NEC).

Katika taarifa yake ilisema Clouds TV na Clouds redio siku ya jumatano Agosti 26 kupitioa kipindi chake cha 360  vimevunja sheria ya uchaguzi ya mwaka 2015 .

Kama sehemu ya adhabu walitakiwa kuomba radhi kw amasaa yaliobaki kabla ya kuanza kifungo Agosti 28

Tume ya taifa ya uchaguzi ilisema kituo kilitangaza matokeo yanaonesha mmoja ya wagombea amepita bila ya kupingwa baada ya  wagombea wengine kushindwa kukizi vigezo vya kikatiba.

Lissu aahidi bima za afya nchi nzima
Shinyanga, Geita vinara wa RAMLI