Timu za Coastal Union na Mtibwa Sugar zimefanikiwa kubaki Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu ujao 2021-22.

Timu hizo zimebaki kwenye Mshike Mshike wa Ligi Kuu, kwa kushinda michezo ya hatua ya Mtoano (Play Off) dhidi ya timu za Ligi Daraja la Kwanza Pamba FC na Transit Camp.

Coastal Union ilicheza nyumbani Uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga, mchezo wa mkondo wa pili hatua ya mtoano (Play Off) na kushinda mabao 3-1.

Ushindi huo umeiwezesha Coastal Union kufikia leo la kuendelea kuwa sehemu ya tinu za Ligi Kuu msimu ujao 2021-22, kwa jumla ya mabao 5-3, kufuatia mchezo wa mkondo wa kwanza kushuhudia timu hizo zikifungana mabao 2-2.

Mkoani Morogoro katika Uwanja wa Jamhuri Mtibwa Sugar imekubali kufungwa bao 1-0 na Transit Camp.

Hata hivyo ushindi huo haujaisaida Transit Camp, kwani kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Dar es salaam Uwanja wa Uhuru, timu hiyo ilipoteza kwa kufungwa 4-1.

Kumbe chanzo ni Kocha Nabi!
Dkt Mpango ashiriki misa ya kumbukizi ya Hayati Mkapa