Klabu ya Coastal Union imeitisha Simba SC kuelekea mchezo wa kesho wa Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’, utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Coastal union ambayo haifanyi vizuri katika Michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara, imetoa tambo hizo baada ya kuwasili jijini Dar es salaam, tayari kwa mchezo huo utakaoanza mishale ya saa moja usiku.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino wa Coastal Union Jonatham Tito amesema, dhamira yao kuu msimu huu ni kutwaa ubingwa wa ‘ASFC’, baada ya msimu uliopita kutimiza jukumu la kucheza fainali na kupoteza mbele ya Young Africans kwa changamoto ya mikwaju ya Penati.

“Malengo yetu Msimu uliopita ilikua ni kucheza Fainali kwenye michuano hii, ambapo tulifanikiwa kwa asilimia 100, Msimu huu malengo yetu ni kutwaa ubingwa wa Michuano hii.”

“Tupo tayari kupambana na Simba SC kesho, tumejiandaa vizuri na tunaamini hilo linawezekana na Mashabiki wao watashangazwa na kitakachowakuta Kwa Mkapa,”

“Tunaifahamu vizuri Simba SC, haitutishi kwa sababu sisi tuna kikosi bora kuliko wao, ninaamini baada ya dakika 90 hili litadhihirika kwa kila mmoja atakaefuatilia mchezo wetu kesho.” amesema Tito

Mayele aitaka Robo Fainali Afrika
Amir Maftah: Sawadogo apewe muda kwanza